Showing posts with label Udaku. Show all posts
Showing posts with label Udaku. Show all posts

Thursday, April 23, 2015

FRENCH MONTANA NA NDINGA MPYA YA BEI HATARIIIII

Mtu mzima wa pande za mbele U.S.A, French Montana wiki amenunua ndinga mpya yenye thamani ya dola million 2.5. Ndinga hiyo kwa siku ya jana, mtu mzima FRENCH alikuwa ameitupiatupia picha zake kwenye ukurasa wake wa fb. Picha hizo zimemuonyesha mtu mzima FRENCH MONTANA akiwa na marafiki zake wakiwa wamepiga picha na gari hilo kwenye mapozi tofauti tofauti.

Thursday, February 26, 2015

NOMA SANA, HII NDO BAISKELI YA MITI YENYE KILA KITU KAMA BAISKELI NYINGINE


Baiskeli hii ni noma sana, imetengenezwa na mtu ambaye pia ni noma kwa kufikiria duuh ni hatari sana. Inasadikiwa kuwa baiskeli hii ina uwezo kukimbia kama baiskeli nyingine bila ya kuharibika kitu chochote. Pia baiskeli hii ni ya gia kwa hiyo kwenye mlima hakuna haja ya kushuka kazi yako wewe ni kubadili tuu gia ili iendane na maeneo iliopo. Duuh!!! ubunifu ni noma sana, Nawe kuwa mbunifu.

Sunday, February 8, 2015

WIZ KHALIFA KUMFUNDISHA DIDDY KUSMOKE WEED


Mtu mzima Wiz Khalifa ameamua kumfundisha besti wake wa karibu DIDDY jinsi ya kuvuta WEED. Juzi kati mtu mzima Diddy alipost kwenye ukurasa wake wa Facebook kw kumpongeza mu mzima Wiz Khalifa kwa kumfundisha kuvuta WEEDY.

Mabesti wa karibu wa Wiz Khalifa walisema kwamba, Mtu yeyote atayekuwa karibu na Wiz bhasi ni lazima afundishwe kuvuta WEEDY kwa sababu WEEDY ndio starehe kubwa ya Wiz maishani kwake. Pia mabesti hao waliongezea kwa kusema kwamba, siku Wiz akiwa na furaha sana huweza kuvuta WEEDY zaidi ya kilo Mbili.

Thursday, February 5, 2015

FROLA MBASHA AFUNGUKA KUHUSU MTOTO ALIYEJIFUNGUA

Msanii wa Injili Frola Mbasha, amefunguka kuwa mtoto aliyejifungua ni mtoto wa mumewe Emmanueli Mbasha na wala sio mtoto wa mchungaji Gwajima. Frola Mbasha amesema kuwa, anataka watu wajue kuwa mtoto wa ni wa mumewe kwa hiyo wasizushe habari wasisizo zijua. Frola Mbasha pia amesema kwamba, hawezi kuzungumzia chochote kuhusu mumewe kwani mumewe kwa sasa ana jeuri ya pesa ndo inayomchanganya".

Sunday, January 18, 2015

DUUH!!! KUMBE NDOMANA RICK ROSS KAFANYA KAZI NA K-MICHELLE

Inasadikiwa kwamba sababu iliyomfanya  mtu mzima Rick Ross kufanya kazi na mwanamziki K-Michelle ni kwa sababu ya umbo la mwanadada huyo. Duuh!! majarida mbalimbali nchini America yalimnukuu Rick Ross baada ya kuulizwa ni kitu kilimvutia hadi akafanya kazi na K-Michelle kwenye nyimbo kali iliyotengenezwa na producer mahiri duniani Timbaland (IF THEY KNEW) ndio akasema "Umbo la K-Michelle ndo lilimchanganya hadi akaamua kupiga nae song kama kumbukumbu duniani"


Tuesday, November 25, 2014

JAGUAR KUTUA BONGO KUMUONA IRENE UWOYA

Msanii kutoka Kenya Jaguar ameweka nia ya kuja bongo kumuona Irene Uwoya kabla ya mwaka huu kuisha.
Jaguar pia amefunguka kuwa hatokuja kumuona tuu Irene Uwoya bali pia ataenda kuwaona wazazi wake Irene kwani anamkubali sana mtoto wao Irene.

DIAMOND KUMUOA ZARI THE BOSS LADY

Marafiki wa karibu wa Diamond na Zari the boss lady wamechonga kimtindo na baadhi ya waandishi wa habari kuwa, mtu mzima Diamond na Zari the boss lady wanatarajia kufunga ndoa mwezi ujao.
Harusi hiyo ambayo wanasema kwamba haitoweza kufanyika Tz wala Ug ila wanampango wa harusi hiyo kwenda kufanyika mbele (mamtoni) kimtindo mtindo kwenda kula bata na wanyamwezi wa mbele.
"Hayo ndo yaliyojiri, so mtu mzima kama vipi nawe anza kujichanga tuelekee mbele kwenye harusi ya mshikaji na goma lake".
(Haya maneno yaliyowekewa fungua semi " na funga semi " yamenukuliwa kutoka kwa rafiki mmoja wa diamond alipokuwa anahojiwa kimtindo na baadhi ya waandishi wa udaku)

Monday, November 24, 2014

PICHA YA DIAMOND AKIBADILISHANA MATE NA ZARI THE BOSS LADY

Duu Yameongelewa Mengi Wengine wakisema ni wapenzi wengine wakikataa na kusema ni Project ya mziki wanafanya pamoja ..Ila hii Picha inaelezea Yote ..Unachoona Ndio Hicho Kubali ama kataaa.. Duuh hilo ndo goma la jipya kwa Diamond duuh!!!!