Saturday, November 15, 2014

ASHUSHWA KWENYE NDEGE KISA UZITO WAKE

Kijana Sande Mrema mwenye tatizo la uzito wa kilo 250 na umri wa maiaka 25 ameshindwa kusafiri kwenda nchini india katika matibabu yake baada ya kushushwa mara kadhaa kwenye ndege za kimataifa anazotakiwa kusafiria licha ya ndugu zake kulipa Gharama zote za usafiri wake.

Aidha kwa maelezo wanayoambiwa na wahusika wa ndege hizo ni kwamba, "mwili wake ni mzito sana hivyo ndege ya abiria haiwezi kuhimili uzito wake kwani itafanya ndege iwe inaelemea upande ambao atakuwa amekaa. Pia wafanyakazi wa ndege hizo wamesema kwamba labda kijana huyo anaweza kupanda ndege ya mizigo kwani, ndege za mizigo huimili uzito mkubwa zaidi ya wake".

No comments:

Post a Comment