Mtoto mmoja wa pande za kishua a.k.a Masaki siku ya juzi aliwagombanisha wazazi wake baada ya kuagizwa na mama yake kumpigia simu baba yake. Mazungumzo hayo kati ya mama na mtoto yalikuwa hivi:
MAMA: Mwanangu embu mpigie simu baba yako kwa sababu, muda mfupi uliopita alinipigia na kuniambia kuwa nimpigie nikiwa nimeshamaliza kupika chakula.
MTOTO: Sawa mama.
Bhas yule mtoto akafanya kama alivyoambiwa na mama yake. Mara mtoto akatoa majibu kwa mama yake.
MTOTO: Mama!!! nimempigia baba, ila hajapokea yeye.
MAMA: khah!! amepokea nani mwanangu??
MTOTO; Amepokea mwanamke mama.
MAMA: Bhas mwanangu hilo swala niachie mimi.
Bhas yule mama na mtoto wake wakaendelea kula chakula. Baada ya muda kidogo wakasikia mlinzi akifungua geti na sauti ya gari. Bhas yule mama alienda mlangoni huku akiwa ameshikilia mwiko, upawa, sufuria, frampeni, vijiko na bila kusahau uma.
Mara baba wa mtoto akafungua mlango, lakini kabla ya kumalizia kuingia ndani, baba wamtoto alishangaa anapigwa na mwiko, upawa , sufuria na vinginevyo huku mama wa mtoto akisema, "utanieleza leo, aliyepokea simu yako ni nani". Mara mama akamwita mtoto wake,:
MAMA: Mwanangu embu mwambie baba yako kuhusu yule mwanamke aliyepokea simu alikuambiaje?
MTOTO: Baba, Yule mwanamke aliyepoke simu alisema kwamba, " Namba unayopiga kwa sasa haipatikani, tafadhali jaribu tena baadae.
Bhas yule mama akachoka akawa hoii na baba wa mtoto nae akawa hajasema kitu.
ASANTE KWA KUSOMA STORI HII AMBAYO IMeKUFURAHISHA. TAFADHALI ENDELEA KUPITIA www.justbehappy005.blogspot.com KWA STORI NYINGINE ZAIDI.
ASANTENI
No comments:
Post a Comment