duuh!!! uswahilini kuna vituko. Mama mwenye nyumba mmoja wa pande za kitaa fulani humu dsm, amempiga mumewe (baba mwenye nyumba) baada ya kukanyaga sehemu aliyokuwa anapiga deki. Watu walioona tukio hilo waliamua kupiga simu polisi, mara moja nao polisi waliwasili kwa muda maalum. Mazungumzo kati ya mama huyo na polis hao yalikuwa hivi:
POLISI; Mama mwenye nyumba, tumepigiwa simu na watu waliokuona una mpiga mume wako (baba mwenye nyumba) kwa hiyo unaweza kutuambia sababu ya kumpiga mume wako??
MAMA MWENYE NYUMBA: Ndio nimempiga kwa sababu amekanyaga sehemu niliyopiga deki ambayo ilikuwa haijakauka.
POLISI: Bhas mama una makosa hivyo unahitajika kituoni.
Mama mwenye nyumba akawa hajajibu. Bhas polisi walimpigia mkubwa wao na kumwambia yaliyotokea.
Mazungumzo ya polisi na mkubwa wao yalikuwa hivi:
POLISI: Afande tupo huku kwenye tukio maeneo ya uswahilini huku, mama mwenye nyumba amempiga mumewe.
AFANDE: Kampiga mumewe kisa nini??
POLISI: Kampiga kisa alikanyaga sehemu aliyopiga deki ambayo ilikuwa haijakauka.
AFANDE: Mmeshamkamata?
POLISI: Hapana afande.
AFANDE: Kwa nini sasa?
POLISI: Tunaogopa kupigwa afande, hivyo tunangojea pakauke ndo tumkamate.
No comments:
Post a Comment