Wednesday, November 19, 2014

NYATI AJERUHI WATU WANNE WILAYANI NAMTUMBO

Watu wanne kutoka kijiji cha Namabengo wilaya ya Namtumbo wamejeruhiwa na nyati na kusababishiwa kulazwa katika kituo cha afya Namabengo mkoani Ruvuma.

Kamanda wa police mkoa wa Ruvuma Mihayo Msekhela amesema watu waliojeruhiwa walikuwa katika shughuli zao za kawaida za kupalilia makaburi,wengine kuloweka mihogo bila kujua ndipo walipovamiwa na Nyati.

Kamanda wa Police Mihayo Msekhela amesema Jeshi la Police lilipo pata taarifa hiyo lilichukua hatua mara moja na kushirikiana na askari wa wanyama Pori kumsaka Nyati huyo hatimaye kuweza kumuua.

No comments:

Post a Comment