Harusi moja iliyofanyika huko nchini Nigeria iliwaacha watu midomo wazi baada ya kuona keki ya shughuli hiyo kufanana kabisa na bi harusi bila hata kukosea kitu hata kimoja.
Keki hiyo inayotathimiwa kuwa ndio keki ya gharama kubwa ambayo haijawahi kutokea nchini humo kuwa imegharimu dola za kimarekani 17000 sawa na milioni kama thelathini hivi za kitanzania.
Tajiri huyo ambaye alifunga ndoa yake miezi kadhaa iliyopita alisema kwamba alitaka kufanya ndoa yake iwe ya kipekee nchini humo, na ndio imekuwa harusi ya kipekee kutokea nchini humo.
No comments:
Post a Comment