Zifuatazo ni hatua chache za kuuleta mwili wako kuwa huru:
1) Kila uamkapo asubuhi salama hakikisha kuwa unapiga push up hqta kumi(10) kwa wavulana ila kwa wasichana hakikisha pia unaruka kamba hara mara kumi (10), kwa kufanya hivi misuli ya mwili wako itaimarika mara dufu na kukufanya uwe huru na mwili wako.
2) Mazoezi ya jogging (kukimbia) ni mazoezi mazuri yanayofanya mtu aweze kupata pumzi zaidi ambayo itaweza kumsaidia kwenye mambo mbalimbali.
Mazoezi ya kukimbia yanafaa muda wa asubuhi au jioni kwa sababu mida hiyo huwa mazingira yametulia tulia.
3) Je, unayafahamu mazoezi ya Aerobics?
Mazoezi ya Aerobics ni mazoezi ya viungo ambayo pia unaweza kuyafanya ukiwa hata nyumbani kwako. Mara nyingi mazoezi ya Aerobics huitaji uwe na mbao (kama step ya ngazi) ambayo ipo kwenye shape ya mstatili ili uweze kufanya aina nyingi za mazoezi kutokana na mbao hiyo.
Kwenye mbao hiyo kuna zaidi ya mazoezi mia moja (100) ambayo yatakufanya uwe huru na mwili wako.
Tafadhali fuatilia hizo steps hapo juu nyinginezo nitazidi kuwatumia ili muwe huru na miili yenu.
Asanteni!!!!!!!!!
No comments:
Post a Comment