Serikali ya Jamuhuri ya watu wa China imehaidi kuisadia Tanzania katika sekta ya kilimo kwa kutoa mafunzo bora na kutafuta masoko kwa ajili ya mazao yatokanayo na kilimo hicho.
Balozi wa china nchini Lu Youqing amesema hayo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro katika maadhimisho ya siku ya Kilimo ya China yaliyofanyika katika kituo cha Utafiti wa Kilimo Bora cha Dakawa Wilayani Morogoro.
Serikali ya China nchini inasema itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa lengo la kuwainua wakulima wadogo nchini ili waweze kuongeza uzalishaji wa mazao na kutawatafutia masoko yenye uhakika ndani na nje ya nchi.
Serikali mkoani Morogoro imesema kupitia mafunzo hayo yanayotolewa na watalaamu kutoka China yatasaidia kuongeza uzalishaji wa mazao ya mpunga na Mahindi nchini.
No comments:
Post a Comment