Mwanamuziki wa zamani wa Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’, Khamis Kayumbu maarufu kama 'Amigolasi' amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa siku kadhaa.
Amigo alilazwa Muhimbili kwa matatizo ya moyo ambapo taratibu za kufanyiwa upasuaji zilikuwa zikiandaliwa lakini mauti yakamkuta kabla ya lolote kufanyika.
Akiwa Twanga Amigo akajijengea umaarufu wa aina yake na akafanikiwa kutunga wimbo mmoja 'AMINATA' ambao ulikamata chati kwa miaka mingi tangu ulivyorekodiwa mwaka 2003.
Msiba uko nyumbani kwa mama mzazi wa marehemu Mburahati jijini Dar es Salaam jirani kabisa na Shule ya Msingi Mianzini huku taratibu za mazishi zikipangwa. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, Amina
No comments:
Post a Comment