Moto mkubwa ulizuka siku ya jana majira ya saa mbili (2) usiku maeneo ya Kibaha Maili Moja umesababisha hasara kubwa kwani, maduka yaliyoungua ni maduka ya kuuza vitu kwa bei ya jumla.
Chanzo cha moto huo ni duka moja ambalo lilianza kuungua na kusababisha maduka mengine yaliyopo karibu naye kushika moto na kusababisha hasara kubwa kwa wamiliki wa maduka hayo.
Kwa mujibu wa baadhi ya walioshuhudia janga hilo la moto walisema kwamba, walitoa taarifa kwa jeshi la Zimamoto na kusikitika kwamba zimamoto walichelewa kufika eneo la tukio na kusababisha mali nyingi izidi kuungua.
No comments:
Post a Comment