Thursday, November 13, 2014

DAKTARI AKAMATWA

India imemkamata Daktari anayedaiwa kuhusika na vifo vya wanawake 15 na kusababisha wengine zaidi ya 90 kuwa katika hali mbaya kufuatia upasuaji wa kufunga uzazi uliofanyika kwenye kambi moja ya kliniki.

DR. RK GUPTA na Msaidizi wake waliendesha upasuaji huo kwa wanawake 83 katika kijiji cha Pendari katika wilaya ya Bilaspur, jimbo la Chhattisgarh.

Mwanamke wa 14 alikufa jana wakati mwingine alikufa baada ya kufanyiwa upasuasji kwenye kambi nyingine ya pili.

DR. GUPTA ambaye mapema alisifiwa na serikali ya jimbo hilo kwa oparesheni zakeza kufunga uzazi kuzuia ongezeko la watu alifanya upasuaji wa kufunga uzazi kwa wanawake 83 kwa muda wa saa tano wakati kanuni zinataka awafanyie wanawake 35 kwa siku moja.

No comments:

Post a Comment