Wednesday, November 5, 2014

BREAKING NEWS: MTOTO ACHANWACHANWA NA VIWEMBE

Mtoto mwenye umri wa miaka 11 Jafari Mashaka mkazi wa Morogoro amechanwachanwa na viwembe miguuni, mikononi kisha kupigwa na mama yake mdogo, kwa sababu ya tuhuma ya kuiba kiasi cha shilingi 4500/=.

Mama yake mdogo huyo aitwaye Tausi Omary alipokuwa anahojiwa ana polisi mkoani humo alikiri makosa na kuomba msamaha kwa kusema kuwa shetani alimpitia.

Taus Omary wamemrudisha rumande mpaka hapo hatima yake itakapo julikana kwani askari polisi bado wanawasubiri wazazi wa mtoto huyo.

No comments:

Post a Comment