Thursday, April 23, 2015

JAMAA APIGWA NA MKEWE KISA MCHEZO WA KUBET

Jamaa mmoja wa pande za Magomeni siku ya juzi alijikuta akipata mkong'oto wa hatari  kutoka kwa mkewe baada ya kisa kuwa, jamaa huwa anaenda kushinda kwenye kubet tuuu bila ya kumwachia mkewe hata hela ya chakula. Hata hivyo kwa habari za majirani wanadai kwamba walishindwa kumtoa jamaa kwenye mkong'oto wa mkewe kwa sababu, mke wa jamaa ananyanyua vyuma hivyo nao wameogopa kuwa nao wangepata mkong'oto kutoka kwa mwanadada huyo.

No comments:

Post a Comment