Bondia wa nchini Tanzania Thomas Mashari amefanikiwa kumpiga mpinzani wake kutoka Kenya bondia Henry Wandela, baada ya kumtufua kwa mikwaju ya usoni mikali ambayo ilimsababishia bondia Thomas kupata point nyingi ambazo zimempa ushindi.
Hapo awali bondia Thomas Mashari alivyokuwa akihojiwa na baadhi ya televisheni nchini alisema ni lazima atampiga mpinzani wake bondia Henry kutoka nchini Kenya. Mungu amemsaidia Thomas Mashari kupata ushindi.
Hongera bondia Thomas Mashari kwa ushindi uliotuahidi watanzania juu ya mchezo wako dhidi ya bondia Henry Wandela kutoka nchini Kenya.
N:B Picha ya hapo juu ni picha inayomuonesha bondia Thomas Mashari akiwa na mwalimu wake.
No comments:
Post a Comment