Naibu katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema Mhe.John Mnyika ameitaka serikali kuacha kutumia mswada wa baraza la vijana kama fursa ya kwenda kinyume na maoni ya wananchi kwa kutaka vijana waikubali katiba inayopendekezwa licha ya upatikanaji kutofuata sheria na kanuni.
Akifungua mkutano wa kamati tendaji ya baraza la vijana la chadema, Mhe.Mnyika amewata vijana kutambua kuwa hakuna mahusiano yeyote kati ya kuanzishwa kwa baraza la vijana la taifa na katiba inayopendekezwa na kusisitiza tanzania kwa sasa haiongozwi na katiba inayopendekezwa.
No comments:
Post a Comment