Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa amesema anafurahishwa na watu wenye maono na wanaopenda kuchukua maamuzi kuliko wale wenye kaliba ya kutaka kuweka rekodi pekee. Katika uzinduzi huo, Lowassa amesema kuwa hakwenda kutangaza nia na bado hajafikia maamuzi hayo, wakati ukifika ataweka wazi nia yake ya kugombea Urais mwakani.
Mh. Lowassa amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa Helkopta ambayo ni mali ya Kanisa la Ufufuo na Uzima lililo chini ya Askofu Josephat GWAJIMA ambayo mbali ya shughuli za kikanisa, itatumika pia katika shughuli mbalimbali za kibinadamu wakati wa majanga.
No comments:
Post a Comment