Thursday, April 23, 2015

JAMAA APIGWA NA MKEWE KISA MCHEZO WA KUBET

Jamaa mmoja wa pande za Magomeni siku ya juzi alijikuta akipata mkong'oto wa hatari  kutoka kwa mkewe baada ya kisa kuwa, jamaa huwa anaenda kushinda kwenye kubet tuuu bila ya kumwachia mkewe hata hela ya chakula. Hata hivyo kwa habari za majirani wanadai kwamba walishindwa kumtoa jamaa kwenye mkong'oto wa mkewe kwa sababu, mke wa jamaa ananyanyua vyuma hivyo nao wameogopa kuwa nao wangepata mkong'oto kutoka kwa mwanadada huyo.

FRENCH MONTANA NA NDINGA MPYA YA BEI HATARIIIII

Mtu mzima wa pande za mbele U.S.A, French Montana wiki amenunua ndinga mpya yenye thamani ya dola million 2.5. Ndinga hiyo kwa siku ya jana, mtu mzima FRENCH alikuwa ameitupiatupia picha zake kwenye ukurasa wake wa fb. Picha hizo zimemuonyesha mtu mzima FRENCH MONTANA akiwa na marafiki zake wakiwa wamepiga picha na gari hilo kwenye mapozi tofauti tofauti.